Jarida la Mapishi

Smoothie ya blueberry na karanga

 • Maandalizi
  Dakika 10
 • Kupika
  -
 • Walaji
  2

Smoothie ya blueberry na karanga, ni smoothie nzuri ambayo yafaa kunywa kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi. Pia unaweza kunywa smoothie hii pamoja na kitafunio chochote kile ukipendacho. Ili kuongeza ladha zaidi, unaweza kutumia asali badala ya sukari katika smoothie hii. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza smoothie hii ya blueberry na karanga.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, maziwa, mtindi, matunda ya blueberry, ndizi, unga wa kitani, siagi ya karanga, pamoja na asali, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Mimina smoothie kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *