Jarida la Mapishi

Lemonade ya blackberry na minti

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  -
 • Walaji
  2

Lemonade ya blackberry na minti, ni kinywaji cha kuburudisha ambacho hutengenezwa kwa kusaga pamoja matunda ya blackberry, majani ya minti na limao. Kinywaji hiki chafaa kunywa katika msimu wa kiangazi, hasa kwenye sherehe. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza lemonade hii ya blackberry na minti.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, limao, apple, matunda ya blackberry, majani ya minti, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Chukua chujio, kisha chuja lemonade hiyo vizuri.

  Step3

  Mimina lemonade kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.

  Conclusion

  Unaweza kuongeza maji zaidi, endapo utaona maji yaliyomo katika lemonade hii ni kidogo.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *