Jarida la Mapishi

Mkate wa machungwa na chocolate

Mkate wa machungwa na chocolate | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 15
  • Kupika
    Dakika 45
  • Walaji
    10

Mkate wa machungwa na chocolate, ni mkate ambao wafaa kula hasa katika sherehe. Mkate huu ambao ni rahisi sana kupika, unapikwa kwa kutumia chocolate, machungwa yaliyo kamuliwa, maganda ya machungwa yaliyo kunwa, pamoja na chocolate. Waweza kula mkate huu kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi, au kama kitindamlo kwenye mlo wowote ule. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa machungwa na chocolate.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, siagi pamoja na sukari, kisha changanya vizuri. Weka mayai na vanilla extract, halafu endelea kuchanganya.

    Step2

    Weka maganda ya chungwa yaliyokunwa, chungwa, na buttermilk, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema.

    Step3

    Weka unga wa ngano, baking powder, chumvi na dark chocolate chips, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step4

    Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.

    Step5

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40 mpaka 45, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.