Jarida la Mapishi

Mkate wa peasi na karoti

 • Maandalizi
  Dakika 35
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  10

Mkate wa peasi na karoti, ni mkate mtamu ambao unapikwa kwa kutumia karoti zilizokunwa (grated) pamoja na peasi. Utamu wa mkate huu, utamfanya mtu ambaye hapendi matunda ya karoti na peasi, ayapende. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa peasi na karoti.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, unga wa ngano, unga wa ngano ambao hauja kobolewa chumvi, baking powder, mdalasini, tangawizi, iliki pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka yai, mtindi, mafuta ya kupikia, karoti na matunda ya peasi, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step3

  Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.

  Step4

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *