Jarida la Mapishi

Mkate wa nazi na zucchini

Mkate wa nazi na zucchini | Jarida la Mapishi
 • Maandalizi
  Dakika 35
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  10

Mkate wa nazi na zucchini, ni mkate mtamu ambao hupikwa kwa kutumia nazi iliyokunwa, tui la nazi, zucchini iliyokunwa, pamoja na viungo mbali mbali. Mkate huu wafaa kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi, kwenye msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa nazi na zucchini.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, light brown sugar, mafuta ya kupikia, buttermilk, zucchini, pamoja na nazi, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka shayiri, unga wa ngano, baking powder, baking soda, mdalasini na tangawizi, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step3

  Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.

  Step4

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *


  The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.