Jarida la Mapishi

Mkate wa chocolate na ndizi

Mkate wa chocolate na ndizi | Jarida la Mapishi
 • Maandalizi
  Dakika 20
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  10

Mkate wa chocolate na ndizi, ni moja yapo ya mikate mitamu ya ndizi ambao ni rahisi sana kupika. Mkate huu hupikwa kwa kutumia ndizi mbivu, ambazo huchanganywa pamoja na dark chocolate chips. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa chocolate na ndizi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, brown sugar, pamoja na siagi, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka mayai na ndizi na uendelee kuchanganya, halafu weka vanilla extract na buttermilk, kisha changanya vizuri hadi iatakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema.

  Step3

  Weka unga wa ngano ambao hauja kobolewa, cocoa powder, baking soda na chumvi, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *


  The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.