Jarida la Mapishi

Mkate wa limao na zucchini

 • Maandalizi
  Dakika 20
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  12

Mkate wa limao na zucchini, ni mkate mtamu unaopikwa kwa kutumia limao iliyo kamuliwa na maganda yake kukunwa, pamoja na zucchini iliyo kunwa. Mkate huu wafaa kula kwenye msimu wa kiangazi kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi, au hata kama kitafunio cha kawaida. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa limao na zucchini.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, zucchini, maganda ya limao, limao iliyo kamuliwa, mayai, pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka mafuta ya kupikia na vanilla extract, halafu endelea kuchanganya.

  Step3

  Weka unga wa ngano, baking powder, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *