Jarida la Mapishi

Mkate wa machungwa

 • Maandalizi
  Dakika 15
 • Kupika
  Dakika 45
 • Walaji
  10

Mkate wa machungwa, ni mkate rahisi kupika wenye ladha nzuri ya machungwa. Tofauti na mikate mingine, ladha ya mkate huu wa machungwa unatokana na tunda halisi la chungwa lililo kamuliwa pamoja na maganda yake kukunwa. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa machungwa.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, maziwa, sukari, pamoja na mafuta ya kupikia, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka maganda ya chungwa yaliyokunwa, chungwa, vanilla extract, cream cheese, pamoja na siagi, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema.

  Step3

  Weka unga wa ngano, baking powder, chumvi na kungumanga, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40 mpaka 45, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *