Jarida la Mapishi

Mkate wa tangawizi

Mkate wa tangawizi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 15
  • Kupika
    Dakika 45
  • Walaji
    10

Mkate wa tangawizi, ni mkate mtamu unaopikwa kwa kutumia viungo, kama vile tangawizi na mdalasini. Mkate huu wafaa kuliwa kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi, lakini pia waweza kula mkate huu kama kitafunio cha kawaida wakati wowote. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa tangawizi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, unga wa ngano ambao hauja kobolewa, unga wa ngano, chumvi, tangawizi, mdalasini, baking powder na baking soda, maziwa, mayai, buttermilk, mafuta ya kupikia na vanilla extract, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step2

    Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.

    Step3

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40 mpaka 45, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step4

    Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.