-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 50
-
Walaji4
Mchuzi wa viazi na njegere, ni chakula kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia, viazi mviringo, njegere, tomato sauce, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Chakula hiki chawafaa zaidi wale ambao wanapenda kula vyakula vya mboga. Unaweza kula chakula hiki pamoja na wali, chapati au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa viazi na njegere.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.
Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.
Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.
Chukua sufuria la ukubwa wa wastani lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za giligilani, chumvi, tomato sauce, pamoja na nusu ya majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10 mpaka 12, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.
Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka viazi pamoja na njegere, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.
Weka maji halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.
Weka nusu ya majani ya giligilani yaliyobaki pamoja na majani ya uwatu, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.
Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review