Jarida la Mapishi

Mboga ya spinachi yenye viazi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  4

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, spinachi, viazi, maji, pamoja na chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step2

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 15 mpaka 20, au hadi utakapo ona viazi vimeiva.

  Step3

  Koroga mboga hizo kwa kasi ili kuvivunja baadhi ya viazi kwa ajili ya kupata mchuzi mzito kama krimu, kisha epua na uweke pembeni.

  Step4

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu maji vimeiva.

  Step5

  Weka tangawizi pamoja na vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

  Step7

  Weka mbegu za giligilani, garam masala, pamoja na binzari ya manjano, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 zaidi. Epua mchanganyiko huo na umimine kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa spinachi, kisha changanya vizuri.

  Step8

  Funika sufuria hilo, halafu weka ichemke kwenye jiko lenye moto mdogo kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *