Jarida la Mapishi

Mchuzi wa bamia

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 35
 • Walaji
  4

Mchuzi wa bamia, ni mboga tamu inayopikwa kwa kutumia bamia mbichi, vitunguu, nyanya pamoja na viungo. Mboga hii yafaa kuliwa pamoja na ugali wali au hata chapati. Fiata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa bamia.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kikubwa chenye vijiko 2 vya chai vya mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vipande vya bamia kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukivigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona pande zote za vipande hivyo vya bamia vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Epua na uweke pembeni, kisha ondoa vipande hivyo vya bamia kutoka kwenye kikaango, na uviweke pembeni kwenye kontena.

  Step2

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tangawizi, vitunguu swaumu, nyanya, tui la nazi, Tamarind Paste, mbegu za giligilani, pamoja na binzari nyembamba, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step3

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia yaliyobaki na uliweke kwenye jiko lenye moto wa mkubwa, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye mchanganyiko ulio usaga kwenye hilo sufuria, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.

  Step4

  Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Weka binzari ya manjano, chumvi, pamoja na viazi mviringo, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

  Step6

  Weka maji kiasi halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

  Step7

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona viazi vimeiva na mchuzi umekuwa mzito.

  Step8

  Weka bamia ulizo zikaanga halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5 zaidi.

  Step9

  Weka majani ya giligilani halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *