Jarida la Mapishi

Mchuzi wa choroko

Mchuzi wa choroko | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Saa 2
  • Kupika
    Dakika 35
  • Walaji
    4

Mchuzi wa choroko, ni pishi lenye virutubisho vyenye afya tele pamoja na ladha nzuri ambayo inatokana na mchanganyiko wa viungo vilivyomo kwenye pishi hili. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika chakula hiki.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka choroko ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa saa 2. Baada ya saa 2, mwaga maji yote yaliyomo kwenye kontena na kubakiwa na choroko peke yake.

    Step2

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mdalasini, iliki, tangawizi, pamoja na nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step3

    Weka mbegu za giligilani, majani ya uwatu, binzari ya manjano, chumvi, choroko, pamoja na vikombe 4 vya maji, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step4

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona choroko zimeiva.

    Step5

    Weka limao, majani ya giligilani, vitunguu vya kijani, pamoja na garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.