Jarida la Mapishi

Biringanya zenye viazi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 35
 • Walaji
  4

Biringanya zenye viazi, ni chakula kitamu na rahisi kupikaa ambacho unaweza kukipika ndani ya dakika 45 tu. Pishi hili hupikwa kwa kutumia vitunguu maji, nyanya,biringanya, viazi mviringo, pamoja na viungo. Chakula hiki chafaa kula kama mlo wa jioni pamoja na chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biringanya hizi zenye viazi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa mkubwa, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za giligilani, binzari ya manjano, chumvi, biringanya, pamoja na viazi, kisha funika sufuria na upike mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.

  Step2

  Punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15 mpaka 25, au hadi utakapo ona viazi na biringanya vimeiva na kuwa laini. (Koroga mchanganyiko huo kila baada ya dakika 3 au 4)

  Step3

  Weka mango powder halafu koroga vizuri, kisha endelea kupika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 5 zaidi.

  Step4

  Weka garam masala na ukoroge tena vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *