-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 10
-
Walaji4
Bamia za kukaanga, ni mboga tamu na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia, bamia, mtindi, unga wa dengu, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika bamia hizi za kukaanga.
Ingredients
Directions
Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, unga wa dengu, mbegu za giligilani, mbegu za shamari, mbegu za kisibiti, binzari nyembamba, chumvi, pamoja na mtindi, kisha changanya hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vizuri na kuwa mzito na laini.
Weka vipande vya bamia, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya bamia vimeenea vyema viungo.
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango bamia moja moja, hadi utakapo ona zimetosha na kuenea kwenye kikaango, kisha kaanga kwa muda wa dakika 2 mpaka 3, au hadi utakapo ona bamia zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa bamia hizo kwenye kikaango na uziweke pembeni kwenye kontena lenye paper towel, kisha acha zikauke mafuta, kabla ya kula. Rudia hatua hii kwa bamia zilizobaki.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review