-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 50
-
Walaji4
Viazi vyenye uwatu, ni chakula kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia viazi mviringo, majani mabichi ya uwatu, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Chakula hiki chafaa kula katika msimu wa baridi pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika viazi hivi vyenye uwatu.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka majani ya uwatu, kisha pika huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 13 mpaka 18, au hadi utakapo ona majani hayo yamekuwa makavu kabisa.
Weka viazi mviringo, chumvi, pamoja na binzari ya manjano, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.
Weka maji halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 20 mpaka 30, au hadi utakapo ona viazi vimeiva, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review