Jarida la Mapishi

Mchuzi wa adesi

Mchuzi wa adesi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 35
  • Walaji
    4

Mchuzi wa adesi, ni pishi ambalo hupikwa kwa kutumia adesi, vitunguu maji pamoja na viungo vya aina mbali mbali kama vile tangawizi, vitunguu swaumu na binzari nyembamba. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika adesi hizi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, adesi, maji, mdalasini, iliki, vitunguu swaumu, binzari ya manjano, pamoja chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step2

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona adesi zimeiva. Epua na uweke kwenye kontena, kisha funika vizuri kontena hilo.

    Step3

    Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona vitunguu maji vimeiva.

    Step4

    Weka tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step5

    Weka mbegu za giligilani na ukaanga kwa sekunde kadhaa. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye mbaazi, kisha koroga vizuri.

    Step6

    Weka garam masala na ukoroge tena vizuri, kisha pakua kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.