Jarida la Mapishi

Mchuzi wa kunde

Mchuzi wa kunde | Jarida la Mapishi
 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 55
 • Walaji
  4

Mchuzi wa kunde, ni pishi lenye utamu ambao utakufanya uone ya kuwa huli kunde za kutosha. Pishi hili la kunde hupikwa kwa kuchanganya kunde, viungo pamoja na maziwa ya mgando. Kunde hizi zafaa sana kula pamoja na wali, lakini pia unaweza kula pamoja na chakula chochote kile ukipendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kunde hizi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka kunde ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa saa 24. Baada ya saa 24, mwaga maji yote yaliyomo kwenye kontena na kubakiwa na kunde peke yake.

  Step2

  Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, kunde, vikombe 3½ vya maji, pamoja na chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step3

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona kunde zimeiva, kisha epua na uweke pembeni.

  Step4

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, tangawizi, pamoja na vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

  Step5

  Weka nyanya pamoja na majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo oka mchuzi umekuwa mzito.

  Step6

  Weka mbegu za giligilani, majani ya uwatu, pamoja na binzari ya manjano, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

  Step7

  Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga, epua mchanganyiko huu na umimine kwenye sufuria lenye kunde.

  Step8

  Weka sufuria hilo lenye kunde kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha chemsha huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15.

  Step9

  Weka garam masala na ukoroge vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Conclusion

  Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *


  The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.