Jarida la Mapishi

Mchuzi wa maharage

Mchuzi wa maharage | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Saa 1 Dk. 10
  • Walaji
    4

Mchuzi wa maharage, ni chakula kitamu, rahisi kupika na chenye lishe. Maharage haya hupikwa kwa kutumia maharage mekundu pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika maharage haya.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka maharage ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa saa 24. Baada ya saa 24, mwaga maji yote yaliyomo kwenye kontena na kubakiwa na maharage peke yake.

    Step2

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, maharage, iliki, mdalasini, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na vikombe 5 vya maji, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step3

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona maharage yameiva, kisha epua na uweke pembeni.

    Step4

    Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na siagi na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta na siagi vipate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, tangawizi, pamoja na vitunguu swaumu, kosha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde kadhaa.

    Step5

    Weka nyanya pamoja na majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

    Step6

    Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga. Weka mbegu za giligilani, majani ya uwatu, pamoja na garam masala, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye sufuria lenye maharage.

    Step7

    Weka sufuria hilo lenye maharage kwenye jiko lenye moto mdogo, kisha chemsha huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15 mpaka 20, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.