Jarida la Mapishi

Mboga ya karoti na spinachi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 20
 • Walaji
  4

Mboga ya karoti na spinachi, ni pishi rahisi kupika ambalo hupikwa kwa kutumia spinachi, karoti, nyanya, pamoja na viungo. Mboga hii yafaa kuliwa pamoja na mkate, chapati, wali au hata ugali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya spinachi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba pamoja na tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona tangawizi imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step2

  Weka karoti, mbegu za giligilani, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

  Step3

  Wela nyanya halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na upike mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona karoti zimeiva.

  Step4

  Weka spinachi halafu koroga vizuri, kisha funika tena sufuria na upike mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona spinachi imenyauka.

  Step5

  Nyunyizia garam masala na ukoroge vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *