Jarida la Mapishi

Magimbi ya kuoka

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 50
 • Walaji
  4

Magimbi ya kuoka, ni kitafunio kitamu chenye ladha nzuri. Tofauti na magimbi mengine, magimbi haya ya kuoka hupikwa kwa kuchanganya pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika magimbi haya ya kuoka.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria magimbi pamoja na maji, kisha chemsha magimbi hayo kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona yameiva. Epua magimbi hayo na uyaweke pembeni ili yapoe. Magimbi yakishapoa, menya maganda yake yote na uyakate katika vipande vidogo vidogo.

  Step2

  Chukua sinia la kuokea. Weka kwenye hilo sinia, magimbi uliyo yachemsha, mafuta ya kupikia, limao, tangawizi, majani ya giligilani, mbegu za kisibiti, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.

  Step3

  Washa jiko la kuoka na uweke joto la nyuzi 220° C, kisha acha jiko lipate moto. Weka sinia lenye magimbi ndani ya hilo jiko la kuokea na uoke kwa muda wa dakika 20 mpaka 30, au hadi utakapo ona magimbi yamebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.Epua magimbi hayo na uyaweke pembeni.

  Step4

  Nyunyizia Chaat Masala juu ya hayo magimbi halafu changanya vizuri, kisha acha yapoe kabla ya kula.

  Conclusion

  Kumbuka kuyageuza magimbi wakati unayaoka, hadi utakapo ona pande zote zimeiva vizuri.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *