-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 25
-
Walaji4
Mboga ya kabichi na choroko, ni mboga tamu, rahisi kupika na yenye afya, ambayo unaweza kuipika kwa muda mfupi sana wa ndani ya dakika 25 tu. Mboga hii hupikwa kwa kutumia kabichi iliyo katwa katwa, choroko, pamoja na viungo. Unaweza kula mboga hii pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya kabichi na choroko.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, mbegu za uwatu, mbegu za giligilani, majani ya mvuje, pamoja na tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.
Weka kabichi, choroko, pamoja na chumvi, halafu funika sufuria, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.
Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona choroko zimeiva.
Weka majani ya giligilani, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 zaidi.
Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review