Jarida la Mapishi

Maboga ya kusaga yenye komamanga

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 35
 • Walaji
  4

Maboga ya kusaga yenye komamanga, ni chakula ambacho hupikwa kwa kutumia maboga yaliyo sagwa, viungo, pamoja na mbegu za kokamanga zilizo kaushwa na kusagwa. Mbegu za komamanga ambazo huwekwa katika chakula hikiz husaidia kuongeza ladha na kukifanya chakula hiki kiwe kitamu zaidi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika maboga haya ya kusaga yenye komamanga.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za uwatu, pamoja na mbegu za giligilani, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

  Step2

  Weka maboga, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona maboga yamebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step3

  Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka maji, kisha funika sufuria na uache ichemke huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona maboga yameiva na kuwa laini.

  Step4

  Weka sukari, mbegu za komamanga, pamoja na majani ya minti, halafu koroga vizuri, kisha funika tena sufuria. Epua na uweke pembeni itulie kwa muda wa dakika 30 mpaka 40, kabla ya kula.

  Conclusion

  Kumbuka kupasha moto maboga hayo, kabla ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *