Jarida la Mapishi

Smoothie ya shayiri na strawberry

 • Maandalizi
  Dakika 5
 • Kupika
  -
 • Walaji
  2

Smoothie ya shayiri na strawberry, ni smoothie tamu inayo tengenezwa kwa kusaga pamoja, shayiri, matunda ya strawberry, ndizi mbivu, soy milk, pamoja na vanilla extract. Smoothie hii yafaa kunywa kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi pamoja na kitafunio chochote kile ukipendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza smoothie hii ya shayiri na strawberry.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, shayiri, matunda ya strawberry, ndizi, soy milk, sukari pamoja na vanilla extract, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Mimina smoothie kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *