Jarida la Mapishi

Lemonade ya kiwi

Lemonade ya kiwi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    -
  • Walaji
    2

Lemonade ya kiwi, ni kinywaji kitamu na cha kuburudisha ambacho hutengenezwa kwa kusaga pamoja kiwi, maji, malimao na matunda ya apple. Kinywaji hiki chafaa sana kunywa katika msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza lemonade hii ya kiwi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, malimao, matunda ya apple, kiwi, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step2

    Chukua chujio, kisha chuja lemonade hiyo vizuri.

    Step3

    Mimina lemonade kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.

    Conclusion

    Unaweza kuongeza maji zaidi, endapo utaona maji yaliyomo katika lemonade hii ni kidogo.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.