Jarida la Mapishi

Lemonade ya karoti

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  -
 • Walaji
  2

Lemonade ya karoti, ni kinywaji kizuri, cha kuburudisha na chenye afya, ambacho hutengenezwa kwa kusaga pamoja karoti na malimao. Lemonade hii yafaa sana kunywa kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza lemonade hii ya karoti.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, malimao, matunda ya apple, karoti, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Chukua chujio, kisha chuja lemonade hiyo vizuri.

  Step3

  Mimina lemonade kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.

  Conclusion

  Unaweza kuongeza maji zaidi, endapo utaona maji yaliyomo katika lemonade hii ni kidogo.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Recipe Reviews

  • Noela

   Asante sana Kwa MAARIFA,Nina swali,lmao umeliosha na kuliweka na maganda yake au umekamua juisi yake ukaiweka kwenye apple na karoti ndani ya Brenda? Asante

   • Mary Joachim

    Unaweza ukamenya limao maganda yake yote kama chenza kisha ukalikata kata na kuliweka kwenye blender, au unaweza kulikamua limao na juisi yake ukaiweka kwenye blender.

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *