-
Maandalizi-
-
Kupika-
-
Walaji2
Lemonade ya kiazisukari, ni kinywaji kizuri na chenye afya, ambacho hutengenezwa kwa kutumia kiazisukari chekundu, malimao, matunda ya apple na maji. Kiazisukari chekundu ni mmea uliosheheni virutubisho vingi vya chuma pamoja na viondoa sumu mwilini, ambavyo ni muhimu sana katika mwili wako. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza lemonade hii ya kiazisukari.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, malimao, matunda ya apple, kiazisukari chekundu, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Chukua chujio, kisha chuja lemonade hiyo vizuri.
Mimina lemonade kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.
Conclusion
Unaweza kuongeza maji zaidi, endapo utaona maji yaliyomo katika lemonade hii ni kidogo.
Leave a Review