Jarida la Mapishi

Keki ya nazi na raspberry

 • Maandalizi
  Dakika 20
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  8

Keki ya nazi na raspberry, ni keki tamu iliyo sheheni ladha ya matunda ya raspberry pamoja na nazi. Keki hii yafaa kuliwa pamoja na chai wakati wa asubuhi au hata wakati wa mchana. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi kupika keki hii ya nazi na raspberry.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, unga wa ngano, nazi iliyokunwa, chumvi, pamoja na baking soda, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Chukua bakuli nyingine ndogo. Weka ndani ya hiyo bakuli, siagi, mafuta ya nazi, sukari, na uchanganye vizuri, kisha weka mayai, pamoja na tui la nazi, halafu changanya tena vizuri.

  Step3

  Chukua mchanganyiko wa bakuli ndogo ya pili, na umimine kwenye mchanganyiko wa bakuli la kwanza. Weka matunda ya raspberry kwenye hilo bakuli la kwanza, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 35 mpaka 40, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *