Jarida la Mapishi

Ice cream ya blueberry na nazi

 • Maandalizi
  Dakika 15
 • Kupika
  -
 • Walaji
  4

Ice cream ya blueberry na nazi, ni ice cream tamu yenye ladha ya mchanganyiko wa matunda ya blueberry pamoja na tui la nazi. Ice cream hii yafaa kula kama kitindamlo katika msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya blueberry na nazi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tui la nazi, matunda ya blueberry, maple syrup, limao, pamoja na vanilla extract, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa saa 1, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

  Step3

  Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *