Jarida la Mapishi

Ice cream ya raspberry

Ice cream ya raspberry | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 10
  • Kupika
    -
  • Walaji
    4

Ice cream ya raspberry, ni ice cream tamu na laini, iliyo sheheni ladha ya matunda halisi ya raspberry yaliyosagwa. Ice cream hii yafaa kula kama kitindamlo katika msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya raspberry.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, matunda ya raspberry, sukari, pamoja na double cream, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

    Step2

    Mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

    Step3

    Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.