Jarida la Mapishi

Ice cream ya cherry

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  -
 • Walaji
  4

Ice cream ya cherry, ni ice cream rahisi sana kutengeza iliyo sheheni ladha ya cherry. Ice cream hii hutengenezwa kwa kutumia matunda ya cherry yaliyo sagwa pamoja na krimu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya cherry.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, matunda ya cherry, sukari pamoja na maziwa, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

  Step2

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena mchanganyiko ulio usaga, double cream pamoja limao, kisha changanya vizuri.

  Step3

  Mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 45, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

  Step4

  Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *