Jarida la Mapishi

Biskuti za mchele

Biskuti za mchele | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 45
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    20

Biskuti za mchele, ni biskuti maarufu na zinazopendwa sana katika nchi ya Iran. Watu wa Taifa hili hupenda kula biskuti hizi za mchele katika sherehe mbali mbali, hasa katika sherehe za mwaka mpya wa Iran. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za mchele.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, siagi, sukari, pamoja na vanilla extract, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka mayai na uchanganye vizuri, kisha weka unga wa ngano, unga wa mchele, baking powder, iliki na chumvi, halafu changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchangayiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step3

    Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.

    Step4

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.