Jarida la Mapishi

Chai ya lozi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 5
 • Walaji
  2

Chai ya lozi, ni chai nzuri na ya kuburudisha ambayo yafayaa sawa kunywewa katika kipindi cha kiangazi (msimu wa joto). Pia waweza kuiandaa chai hii kwa ajili ya wageni wako katika sherehe ya aina yoyote ile. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza chai hii ya lozi

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, maji pamoja na mbegu za shamari, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step2

  Ukiona imeanza kuchemka, mimina maziwa halafu koroga vizuri, kisha acha tena ichemke.

  Step3

  Ukiona imeanza tena kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo. Weka majani ya chai halafu koroga vizuri, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa sekunde 30.

  Step4

  Zima jiko, kisha funika sufuria na uache chai itulie kwa muda wa dakika 2.

  Step5

  Chukua vikombe 2 pamoja na chujio. Weka nusu ya lozi kwenye kikombe cha kwanza, na nusu ya lozi iliyobaki kwenye kikombe cha pili.

  Step6

  Chuja chai ndani ya hivyo vikombe. Weka sukari kadiri ya mahitaji yako, kisha koroga vizuri, tayari kwa kunywa.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *