Jarida la Mapishi

Biskuti za lozi

Biskuti za lozi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Saa 1
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    20

Biskuti za lozi, ni biskuti laini, tamu, na rahisi sana kupika. Biskuti hizi hupikwa kwa kutumia unga wa lozi, almond extract, pamoja na lozi mbichi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za lozi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, sukari, pamoja na almond extract, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka viini vya mayai na uchanganye vizuri, halafu weka unga wa ngano, unga wa lozi, chumvi, baking powder na lozi, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step3

    Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.

    Step4

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.