Jarida la Mapishi

Viazi vitamu vya kuchemsha

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  4

Viazi vitamu vya kuchemsha, ni chakula kizuri chenye afya kilicho sheheni virutubisho vingi hasa Wanga, Vitamini A, Vitamini C, pamoja na Vitamini B6. Viazi hivi hupikwa kwa kuvichemsha pamoja na viungo. Viungo vinavyowekwa katika viazi hivi husaidia kuongeza ladha na kuvifanya viazi hivi viwe vitamu zaidi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika viazi hivi vitamu vya kuchemsha.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi vitamu, maji, pamoja na chumvi, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto mkubwa kwa muda wa dakika 1 mpaka 2. Punguza moto na uweke moto wa wastani kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 zaidi, au hadi utakapo ona viazi vimeiva.

  Step2

  Weka Tamarind Paste pamoja na Chaat Masala na ukoroge vizuri, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 2 mpaka 3, huku ukigeuza geuza viazi mara kwa mara, hadi utakapo ona maji yote yaliyomo kwenye sufuria yamekauka.

  Step3

  Weka majani ya giligilani na upike huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 zaidi, kisha epua na uweke kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *