Jarida la Mapishi

Biringanya za nazi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 45
 • Walaji
  4

Biringanya za nazi, ni mboga tamu ambayo yafaa kupika hasa katika kipindi cha kiangazi. Mboga hii hupikwa kwa kutumia biringanya, nazi, pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biringanya hizi za nazi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, nazi iliyokunwa, tangawizi, vitunguu swaumu, vitunguu maji, mbegu za giligilani, garam masala, pamoja na binzari ya manjano, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

  Step2

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria mchanganyiko ulio usaga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step3

  Weka biringanya, tui la nazi, pamoja na chumvi na ukoroge vizuri, kisha acha ichemke katika moto mkubwa kwa muda wa dakika 4. Punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 20 mpaka 30, au hadi utakapo ona biringanya zimeiva. Kumbuka kufunua sufuria na kukoroga mara kwa mara wakati biringanya zinaendelea kuchemka.

  Step4

  Weka limao, majani ya giligilani, pamoja na majani ya minti na ukoroge vizuri, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 2 mpaka 4 zaidi, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *