Jarida la Mapishi

Mboga ya kauliflawa, karoti na maharage machanga

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  4

Mboga ya kauliflawa, karoti na maharage machanga, ni mboga tamu na rahisi kupika, ambayo unaweza kuipika kwa mfupi sana wa ndani ya dakika 30 tu. Mboga hii hupikwa kwa kutumia kauliflawa, karoti, maharage machanga, vitunguu maji, pamoja na viungo. Mboga hii yafaa sana kula pamoja na wali wa binzari ya manjano, au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya kauliflawa.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za kisibiti, vitunguu maji pamoja na tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

  Step2

  Weka vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

  Step3

  Weka mbegu za giligilani, binzari ya manjano, vikombe vya mboga mchanganyiko, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

  Step4

  Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

  Step5

  Funika sufuria vizuri, kisha pika mboga hizo kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona zimeiva.

  Step6

  Weka white vinegar pamoja na majani ya giligilani, kisha endelea kupika mboga hizo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 zaidi.

  Step7

  Nyunyizia garam masala na ukoroge vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *