Jarida la Mapishi

Smoothie ya peasi

Smoothie ya peasi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 10
  • Kupika
    -
  • Walaji
    2

Smoothie ya peasi, ni smoothie yenye afya, rahisi kutengeneza na iliyo sheheni protini kwa wingi, ambayo hutengenezwa kwa kutumia matunda ya peasi, ndizi, mtindi, maziwa, pamoja na mdalasini. Waweza kunywa kinywaji hiki kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi. Pia waweza kunywa smoothie hii pamoja na kitafunio chochote ukipendacho wakati wowote ule. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza smoothie hii ya peasi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, maziwa, mtindi wa vanilla, peasi, ndizi, pamoja na mdalasini, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step2

    Mimina smoothie kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.