-
Maandalizi-
-
Kupika-
-
Walaji2
Lemonade ya chenza na pichi, ni kinywaji kitamu na cha kuburudisha kilicho sheheni ladha ya uchachu, ambacho hutengenezwa kwa kusaga pamoja chenza, pichi, limao, apple na maji. Kinywaji hiki chafaa sana kunywa katika msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza lemonade hii ya chenza na pichi.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, pichi, limao, apple, chenza, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Chukua chujio, kisha chuja lemonade hiyo vizuri.
Mimina lemonade kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.
Conclusion
Unaweza kuongeza maji zaidi, endapo utaona maji yaliyomo katika lemonade hii ni kidogo.
Leave a Review