Jarida la Mapishi

Juisi ya peasi

 • Maandalizi
  Dakika 10
 • Kupika
  -
 • Walaji
  1

Juisi ya peasi, ni juisi tamu, rahisi kutengeneza na yenye faida nyingi za kiafya, ambayo imesheheni virutubisho vingi vya Vitamini C na Potasiamu. Fuata hatua zifuatazo, ili kujifunza jinsi ya kutengeneza juisi hii ya peasi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Osha vizuri matunda ya peasi kwenye maji yanayo tiririka, kisha menya maganda yake. Kata kila tunda la peasi katika vipande 4, kisha ondoa mbegu zilizomo ndani ya matunda hayo.

  Step2

  Weka vipande hivyo vya peasi kwenye mashine ya kusaga (blender), pamoja na maji, limao, na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko wa juisi umesagika vyema.

  Step3

  Chuja juisi kwa kutumia chujio, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi kabla ya kunywa.

  Conclusion

  Unaweza kuongeza maji kwenye juisi hii kadiri upendavyo, endapo utaona maji yaliyomo katika juisi hii kidogo.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *