Jarida la Mapishi

Muffins za viazi vitamu na zucchini

Muffins za viazi vitamu na zucchini | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 40
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    12

Muffins za viazi vitamu na zucchini, ni muffins tamu ambazo hupikwa kwa kutumia viazi vitamu vilivyo sagwa, pamoja na zucchini iliyokunwa. Muffins hizi zafaa kula kama kitindamlo baada ya mlo wa jioni, au kama kitafunio cha kawaida wakati wowote. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika muffins hizi za viazi vitamu na zucchini.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, viazi vitamu, zucchini, light brown sugar, heavy cream, mayai, mafuta ya kupikia, pamoja na maganda ya limao, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka unga wa ngano, baking powder, baking soda, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step3

    Chukua sufuria la kuoka muffins (muffins pan), lenye matundu 12 ya muffins, na uweke ndani ya hayo matundu karatasi za kuokea muffin (muffin papers). Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka muffins.

    Step4

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka muffins ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona muffins zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Muffins zikisha iva, ziondoe kwenye jiko la kuoka, kisha ziweke pembeni ili zipoe, zikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka muffins. Muffins zikishapoa, unaweza kuzitoa ndani ya sufuria la kuoka muffins, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.