Jarida la Mapishi

Keki ya siagi

Keki ya siagi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 30
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    8

Keki ya siagi, ni keki tamu ambayo asili yake ni kutoka nchini Marekani. Keki hii hupikwa kwa kutumia unga wa ngano, siagi, mayai pamoja na sukari. Keki hii yafaa sana kuliwa kama kitindamlo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya siagi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, sukari, pamoja na vanilla extract, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka mayai, halafu endelea kuchanganya.

    Step3

    Weka unga wa ngano, baking powder, chumvi, pamoja na maziwa, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step4

    Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

    Step5

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Recipe Reviews

    Avarage Rating:
    • 5 / 5
    Total Reviews:( 1 )
    • Clara

      Inasaidia sana wanawake na wanaume kuandaa vyakula vizuri na vyenye kuzingatia afya yaani mlo kamili

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.