Jarida la Mapishi

Ice cream ya chocolate

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  -
 • Walaji
  3

Ice cream ya chocolate, ni ice cream tamu inayo tengenezwa kwa kutumia dark chocolate chips zilizo yeyushwa, maziwa, pamoja na krimu. Ice cream hii yafaa kuka kama kitindamlo, baada ya mlo wowote ule. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya chocolate.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria ndogo. Weka maziwa ndani ya hilo sufuria, kisha acha yachemke kwenye jiko lenye moto wa wastani. Ukiona yameanza kuchemka weka dark chocolate chips kisha, koroga hadi utakapo ona dark chocolate chips zote zimeyeyuka. Epua mchanganyiko huo na uweke pembeni.

  Step2

  Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli, viini vya mayai pamoja na sukari, kisha changanya vizuri. Mimina mchanganyiko huu kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa maziwa, halafu koroga vizuri.

  Step3

  Chukua sufuria kubwa. Weka maji ya moto kwenye hilo sufuria. Weka mchanganyiko wa maziwa ulio uchemsha ndani ya hilo sufuria lenye maji ya moto, kisha changanya kwa kupiga piga mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 10.

  Step4

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli maji ya baridi pamoja na vipande vya barafu (ice cubes). Ondoa sufuria ndogo ulilo liweka ndani ya sufuria kubwa lenye maji ya moto, halafu weka sufuria hilo ndani ya hili bakuli lenye maji ya baridi, kisha koroga mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 10.

  Step5

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena mchanganyiko wa maziwa, kisha funika vizuri kontena hilo na uliweke kwenye friji kwa muda wa saa 1.

  Step6

  Baada ya saa 1, ondoa kontena hilo kwenye friji, kisha mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

  Step7

  Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *