-
MaandaliziDakika 35
-
KupikaDakika 40
-
Walaji10
Mkate wa karanga na ndizi, ni mkate mtamu ambao mtu yoyote anayependa karanga anaweza kuufurahia. Mkate huu hupikwa kwa kutumia siagi ya karanga ambayo huchanganywa pamoja na ndizi na chocolate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa karanga na ndizi.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, unga wa ngano ambao hauja kobolewa, unga wa ngano, mbegu za kitani, baking soda, baking powder, chumvi pamoja na mdalasini, kisha changanya vizuri.
Chukua bakuli nyingine ndogo. Weka ndani ya hiyo bakuli ndizi mbivu, mtindi, siagi ya karanga, mafuta ya kupikia, mayai pamoja na asali, kisha changanya vizuri.
Chukua mchanganyiko wa bakuli ndogo ya pili, na umimine kwenye mchanganyiko wa bakuli la kwanza, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.
Leave a Review