Jarida la Mapishi

Mkate wa maboga na nazi

 • Maandalizi
  Dakika 20
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  10

Mkate wa maboga na nazi, ni mkate mtamu na rahisi kupika, ambao hupikwa kwa kutumia boga lililo sagwa, tui la nazi, nazi iliyokunwa, pamoja na viungo. Mkate huu wafaa kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi katika msimu wa vuli. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa maboga na nazi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, mafuta ya kupikia, mayai, maboga, pamoja na vanilla extract, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka nazi ya unga, nazi iliyo kunwa, chumvi, baking powder, mdalasini na tangawizi, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step3

  Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.

  Step4

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *