Jarida la Mapishi

Mkate wa mdalasini

Mkate wa mdalasini | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 20
  • Kupika
    Dakika 40
  • Walaji
    10

Mkate wa mdalasini, ni mkate mtamu wenye ladha ya vanila na mdalasini. Mkate huu wafaa sana kuliwa pamoja na siagi ya karanga. Pia waweza kuutumia mkate huu kutengeneza Tosti ya Kifaransa. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa mdalasini.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, maple syrup, siagi, mayai, pamoja na maziwa, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka unga wa ngano, chumvi, baking powder, light brown sugar, dark brown sugar, na mdalasini, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step3

    Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.

    Step4

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 35 mpaka 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.