-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 35
-
Walaji4
Viazi vyenye komamanga, ni chakula rahisi kupika chenye mchanganyiko wa ladha ya utamu na uchachu, ambacho hupikwa kwa kutumia viazi mviringo, mbegu za komamanga, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Viazi hivi vyafaa kula katika msimu wa sikukuu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika viazi hivi vyenye komamanga.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.
Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.
Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mbegu za komamanga pamoja na mbegu za giligilani, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka viazi ulivyo vichemsha pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.
Weka majani ya giligilani pamoja na binzari nyembamba halafu kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review