Jarida la Mapishi

Mboga ya kauliflawa

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  4

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa lenye kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka viazi mviringo kwenye hilo sufuria, halafu kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia, kisha epua na uviweke pembeni kwenye kontena.

  Step2

  Weka kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia kilicho bakia kwenye sufuria hilo hilo, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kauliflawa, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step3

  Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka viazi mviringo ulivyo vikaanga mwanzoni, tangawizi, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria, na upike mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15 mpaka 25, au hadi utakapo ona kauliflawa na viazi vimeiva na kuwa laini.

  Step4

  Weka majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 zaidi.

  Step5

  Nyunyizia garam masala na ukoroge vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *