Jarida la Mapishi

Mboga ya karoti na viazi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 20
 • Walaji
  4

Mboga ya karoti na viazi, ni mboga tamu na yenye afya ambayo hupikwa kwa kumia karoti, dengu, viungo, viazi mviringo, pamoja na tui la nazi. Waweza kula mboga hii kula pamoja na mlo wowote wa jioni, kama vile wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya karoti na nazi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, binzari nyembamba, dengu, mbegu za giligilani, chumvi, karoti, viazi mviringo, pamoja na maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 4.

  Step2

  Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na upike mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona viazi vimeiva na kuwa laini.

  Step3

  Nyunyizia limao pamoja na nazi halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *