Jarida la Mapishi

Keki ya strawberry

 • Maandalizi
  Dakika 15
 • Kupika
  Dakika 45
 • Walaji
  8

Keki ya strawberry, ni keki rahisi sana kupika. Keki hii yawezekana ikawa ndio keki tamu kuliko keki zote ulizowahi kupika au kula katika maisha yako. Ulaiji wa keki hii ya strawberry, ni njia moja ya kula na kufaidi faida za kiafya za matunda ya steawberry. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya strawberry.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka mayai, mtindi na vanilla extract, halafu endelea kuchanganya.

  Step3

  Weka unga wa ngano, baking powder, pamoja na matunda ya strawberry, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40 mpaka 45, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *